Sote tuwe na hasira, kwa wenye kutusaliti,
Kijani ndo mazingira, ovyo miti hatukati,
Heri kwenu wana Kenya, HERI-Kenyatuilinde.
Afya nayo iwe Njema, tujuze nayo jamii,
Kenya iwe kama hema, wajae na watalii,
Kama HERI tunasema, Mazingira tuchafuii,
Heri kwenu wana Kenya, HERI-Kenya tuilinde.
Dokta Mutuku hongera, wanzilishi wayo HERI,
Desiree pia hongera, pamoja kwenye safari,
Na wanachama hongera, kuwajibika na Heri,
Heri kwenu wana Kenya,